BETIKA & TIGO – TUSEPE ABIDJAN KI-VIP (“Kampeni”)

Kampeni itafanyika kuanzia tarehe 06 Desemba 2023 hadi tarehe 06 February 2024 isipokuwa kama itafutwa, kuongezwa muda au vinginevyo ("Kampeni").

JINSI INAVYOFANYA KAZI

  • Promosheni hii ni maalum kwa wateja wenye akaunti ya Betika inayotumika kubeti kwa pesa taslimu kutumia Tigo Pesa pekee (wateja wa makampuni mengine ya simu hawatastahili ushindi kwenye kampeni hii).
  • Promosheni hii inapatikana kwenye njia zote za Betika, SMS, USSD, na njia zote za tovuti.
  • Kampeni hii ni mahususi kwa beti za kabla ya mechi na Live na kila ubashiri unaofuzu utastahili zawadi moja tu ya kushinda kwa siku.

VIGEZO NA MASHARTI

  • Kampeni ni maalum kwa bashiri zitakazowekwa kwa pesa taslimu (Bashiri zilizofuzu)
  • Bashiri zilizoghairiwa na zilizofutwa, na mechi zilizoahirishwa hazitastahili ushindi kwenye promosheni hii.
  • Matokeo ya ubashiri, yaani ikiwa mkeka utachanika au kushinda, hayataathiri idadi ya bashiri za mteja zinazostahili ushindi wa zawadi kwenye promosheni hii. Bashiri zote zinazofuzu zitaongezwa kwa hesabu ya mteja yenye kikomo kwa beti moja kwa siku wakati wa Kampeni hii.
  • Kuhusu zawadi.
    • Washindi wa kila siku watapatikana kupitia droo ya bahati nasibu ya kila siku: Washindi 50 wenye bahati watachaguliwa na watapata zawadi ya Tshs 25,000 ambayo itawekwa kwenye akaunti yao ya Betika. Mteja anaweza kushinda zawadi ya kila siku mara moja tu wakati wa kampeni hii.
    • Washindi wa kila wiki watapatikana kupitia droo ya kila wiki, na kutangazwa siku ya Jumatatu, ingawa 'siku inaweza kubadilika'. Washindi wawili wenye bahati watateuliwa kila wiki, na kila mmoja atapata zawadi ya televisheni ya Hisense ya inchi 70 na usaajili wa DSTV wa mwezi mmoja (inaweza kubadilika kulingana na upatikanaji). Betika itatangaza washindi kupitia majukwaa yake mbali mbali ya mitandao ya kijamii, kwa mfano, Instagram na Facebook, Twitter. Mteja anaweza kushinda zawadi ya kila wiki mara moja tu wakati wa kampeni hii.
    • Zawadi kubwa ya VIP itatangazwa tarehe 02 Januari 2024 (siku inaweza kubadilika), ambapo washindi sita watashinda nafasi ya kusafiri na kwenda na kuangalia mechi za Afcon moja kwa moja Ivory Coast (Watastahili ikiwa wanakidhi mahitaji muhimu ya kusafiri Ivory Coast). Mteja anaweza kushinda zawadi ya VIP mara moja tu wakati wa kampeni hii.
  • Timu ya huduma ya wateja ya Betika itawasiliana moja kwa moja na washindi wa zawadi ya kila wiki na zawadi kubwa ya VIP.
  • Wafanyakazi, wawakilishi, mawakala, au washirika wa Betika, pamoja na wanafamilia wao wa karibu, hawastahili kushiriki katika kampeni hii.
  • Endapo kama kutatokea mzozo kuhusu promosheni hii, uamuzi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha ya Tanzania utakuwa wa mwisho.
  • Kwa kushiriki katika kampeni, maana yake wateja wamekubaliana na vigezo na masharti ya kampeni hii na watazingatia na kufungwa na sheria na masharti haya.
  • Zawadi haziwezi kubadilishwa na hazipaswi kubadilishwa na zawadi nyingine mbadala.
  • Fungu kubwa la zawadi ya VIP linajumuisha tiketi ya ndege ya safari ya kwenda na kurudi kutoka Dar es Salaam hadi Abidjian, siku 2 za kulala kwenye Hoteli, Visa, chakula hotelini, tiketi ya mechi ya uwanjani, na usafiri kuingia na kutoka uwanjani. Zawadi kubwa ya VIP ina thamani ya pesa kisichozidi kiwango cha juu cha Tshs milioni 6 kwa kila mshindi mmoja.
  • Washindi watawasiliana na Betika kupitia namba ya simu ya mshindi iliyosajiliwa, ambaye atalazimika kutuma ushahidi wa utambulisho ikiwa pamoja na kuwasilisha mwenyewe kwenye Ofisi za Betika ushahidi wa utambulisho (kitambulisho na picha ya pasipoti) na umiliki wa namba iliyosajiliwa na ikijumuisha nyaraka za uthibitisho kabla ya zawadi yoyote kutolewa. Nyaraka zitakazohitajika kwaajili ya utambulisho ni kama ifuatavyo:
    • Uthibitisho wowote wa utambulisho
    • Kitambulisho cha Taifa
    • Pasipoti kusafiria
    • Kitambulisho cha Mpiga Kura,
    • Leseni ya Udereva,
    • Kitambulisho cha Mfanyakazi, vitambulisho vilivyoidhinishwa au barua kutoka kwa mamlaka ya serikali ya mitaa.
  • Betika ina haki ya kutumia majina, rekodi za sauti zitakazotumika radioni, motion, picha mgando za mshindi wa promosheni kwa lengo la kujitangaza kupitia kampeni za masoko, na usimamizi wa promosheni. Kwa kushiriki katika promosheni maana yake umekubali kwamba Betika na washirika wake wanaweza kutumia maelezo yako kuwasiliana na wewe kuhusu bidhaa zao, huduma na sababu nyingine za kimasoko na promosheni.
  • Betika haitoi dhamana ya upatikanaji wa promosheni kwenye vifaa na njia zote au upatikanaji wake wakati wote.
  • Betika ina haki ya kufuta, kusitisha, kubadilisha, au kusimamisha ofa hii wakati wowote bila taarifa.
  • Vigezo na masharti vya promosheni hii vinaweza kubadilishwa bila taarifa wakati wowote na Betika kwa hiari yake yenyewe.
  • Betika ina haki ya kufuta ushindi wowote, kwa hiari yake, na itachukua hatua stahiki katika hali yoyote ikiwa ni pamoja na:
    • Mfumo au kosa la program; au
    • Kushtakiwa kuwa kuna vitendo vilivyopigwa marufuku vimefanika.
  • Promosheni imetolewa “kama ilivyo”, bila dhamana ya aina yoyote, wa kueleza au kudokezwa, ikijumuisha bila kikomo, dhamana ya jina, kutokiuka, kutoingiliwa, usahihi wa data, usahihi wa tafsiri, upatikanaji, muda, uuzaji. , kufaa kwa madhumuni mahususi, kando na zile dhamana ambazo zinadokezwa na ambazo hazina uwezo wa kutengwa, vikwazo, au marekebisho chini ya sheria zinazotumika kwa vigezo na Masharti na Sera ya faragha ya Jumla ya Betika.